Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Wakili Agape Fue, leo 2 Desemba 2025 amezindua rasmi mafunzo ya siku tano kwa Viongozi wa Jamii za Ujifunzaji (JZE) yanayofanyika katika Ukumbi wa TRC – Pangani.
Mafunzo haya yanayodhaminiwa na Mradi wa Shule Bora yamelenga kuongeza ujuzi kwa Walimu Wakuu wa shule za msingi katika mbinu shirikishi za ufundishaji kulingana na mtaala mpya—ili kuhakikisha watoto wanapata elimu bora, yenye ubunifu na matokeo chanya
Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Wakili Fue ameushukuru Mradi wa Shule Bora kwa jitihada zake za kuboresha elimu nchini, na kusisitiza kuwa mafunzo haya ni hatua muhimu katika kuleta mabadiliko makubwa ya kielimu Wilayani Pangani.

Naye Mwakilishi wa Afisa Elimu Mkoa wa Tanga, Bi. Digna Tesha, amesema mafunzo hayo yataongeza uwezo wa walimu kukabiliana na changamoto za ujifunzaji darasani, na kuimarisha ushiriki wa wanafunzi kwa kuunda mazingira rafiki ya kujifunzia

Walimu washiriki wanatarajiwa kuibuka na ujuzi na mbinu mpya zitakazoongeza ufanisi wa ufundishaji, kupandisha kiwango cha ufaulu, na kuendelea kuliinua taifa kupitia e
limu bora.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa