Leo tarehe 3 Disemba 2025, Shirika la Tanzania Forest Conservation Group (TFCG) kwa ushirikiano na MJUMITA kupitia Mradi wa Suluhisho la Ujumuishaji wa Misitu na Nishati Endelevu – Tungamotaka Tanzania, limekabidhi pikipiki mpya aina ya YAMAHA kwa Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira cha Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.

Lengo kuu la pikipiki hii ni kurahisisha utekelezaji wa shughuli za Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Asili ya Mseko (Beho) na Kwakibuyu (Bojo) pamoja na kulinda na kuhifadhi rasilimali za misitu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho

Makabidhiano hayo yameratibiwa na kushuhudiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wakili Msomi Agape Fue pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira ndugu Twahiru Mkongo
Tukio hilo limefanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Halmashauri Mkoma.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa