Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Pangani lafanya Mkutano wa Robo ya Pili ya Mwaka wa Fedha 2025/2026

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Pangani leo, Januari 23, limefanya Mkutano wake wa Robo ya Pili ya Mwaka wa Fedha 2025/2026 katika Ukumbi wa YMCA, ambapo limejadili utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba.

Akizungumza mara baada ya kufungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mheshimiwa Sefu Ally, amewasisitiza madiwani kusimamia kwa karibu ukusanyaji wa mapato ya ndani, kuongeza vyanzo vipya vya mapato, pamoja na kuhakikisha Halmashauri ina uwezo wa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ufanisi.
Mheshimiwa Sefu ameeleza kuwa mapato ya Halmashauri ni msingi muhimu wa kuboresha utoaji wa huduma za kijamii, hususani katika sekta za elimu, afya na miundombinu.

Aidha, Baraza hilo limepokea na kujadili kwa kina taarifa za kamati ambapo masuala mbalimbali yalipata nafasi ya kujadiliwa yakiwemo masuala ya elimu, upatikanaji wa madarasa ya kutosha, walimu wenye sifa, pamoja na kuboresha mazingira ya kujifunzia ili kuongeza ufaulu na kupunguza tatizo la utoro Shuleni.

Mkutano huo umehitimishwa kwa wito kwa madiwani na watendaji kushirikiana kwa karibu katika kusimamia rasilimali za umma kwa uwajibikaji na ufanisi.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa