Leo tarehe 22 Januari 2026, Baraza la Madiwani limekutana kujadili taarifa za maendeleo ya kata kwa robo ya pili ya kipindi cha Oktoba – Disemba 2025/2026.
Katika kikao hicho, Madiwani wamewasilisha kwa nyakati tofauti maendeleo yaliyofikiwa katika kata zao pamoja na changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi.
Waheshimiwa Madiwani wameishukuru Serikali kwa kutoa fedha zilizowezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo katika sekta za, Afya,
Elimu,Maji pamoja na Miundombinu ya barabara.
Serikali inaendelea kuboresha maisha ya wananchi Wilayani Pangani kupitia miradi ya maendeleo katika kila kata.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa