Ujenzi wa Shule ya Msingi Stahabu Wakamilika, Tayari kwa Matumizi
Leo tarehe 20 Januari 2026, wajumbe wa Kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi wametembelea na kukagua ujenzi wa Shule ya Msingi Stahabu, iliyojengwa na Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Nyati.
Ujenzi wa shule hiyo mpya umefanyika kufuatia kuhamishwa kwa shule ya zamani ili kupisha zoezi la uchimbaji wa madini yaliyogundulika katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa taarifa ya ukaguzi, jumla ya madarasa 16 yamekamilika, pamoja na ujenzi wa Vyoo matundu 14,Ofisi za walimu,Nyumba ya mwalimu mbili kwa moja, na Maktaba.

Aidha Kamati imeridhishwa na ubora wa ujenzi na imethibitisha kuwa shule iko tayari kuanza kutumika rasmi.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa