Katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Halmashauri ya Wilaya ya Pangani leo, tarehe 27 Januari 2026, imefanya zoezi la upandaji wa miti katika Shule ya Sekondari Muhembo kama ishara ya dhati ya kuenzi na kutunza mazingira.

Zoezi hili limebeba ujumbe mzito wa ulinzi wa mazingira, kizazi kijacho na maendeleo endelevu, likiwa ni sehemu ya kuendeleza maono ya Rais wetu ya Taifa la kijani, lenye uhakika wa rasilimali kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Kupitia hatua hii, Pangani inaendelea kuonesha mfano wa vitendo katika kulinda uhai wa ardhi na kuimarisha mustakabali wa nchi yetu.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa