Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mheshimiwa Gift Isaya Msuya, leo tarehe 1 Septemba 2025 amezindua kampeni ya kitaifa ya chanjo ya mifugo katika kijiji cha Mivumoni.
Kampeni hii inalenga kuongeza ulinzi wa mifugo dhidi ya magonjwa mbalimbali yanayoathiri uzalishaji na ustawi wa wafugaji.
Katika uzinduzi huo, Mh. Msuya alisisitiza umuhimu wa wafugaji kushirikiana kikamilifu na wataalam wa mifugo ili kuhakikisha mifugo yote inapata chanjo kwa wakati, kwa lengo la kuongeza tija na kipato cha kaya.
Pia alihimiza wananchi kuzingatia elimu watakayopewa na maafisa mifugo ili kuhakikisha kampeni inafanikiwa.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa