Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mheshimiwa Gift Isaya Msuya leo Oktoba 11, 2024 amezindua rasmi zoezi la Kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga kura na kutumia fursa hiyo kujiandikisha pia.
Mhe Gift Isaya Msuya amefanya zoezi hilo katika kituo cha Mkoma, Wilayani Pangani ambapo ametumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi kuendelea kutumia haki yao ya msingi kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kujiandikisha katika zoezi hili muhimu.
Ikumbukwe kuwa zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga Kura litafanyika kwa muda wa siku 10 kuanzia leo 11 hadi 20 Oktoba,2024.
" Serikali za Mitaa Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi".
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa