Mashindano ya Michezo ya Ardhi Tanga Yazinduliwa Rasmi Pangani
Leo, tarehe 14 Septemba 2025, Katibu Tawala wa Wilaya ya Pangani, Bi. Ester Gama, amezindua rasmi Mashindano ya Michezo ya Ardhi Tanga yanayodhaminiwa na shirika la World Vision Tanzania.
Mashindano hayo yamekusudia kuhamasisha jamii kuhusu utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati safi kama njia ya kulinda ardhi na rasilimali kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Katika uzinduzi huo, Bi. Gama alipata fursa ya kushuhudia mchezo wa kwanza kati ya timu ya Madanga na Jaira, uliofanyika katika uwanja wa Jaira, ambapo Timu ya Jaira iliibuka na ushindi wa goli 5–2.
Bi. Gama alisisitiza umuhimu wa michezo si tu kwa afya na mshikamano wa jamii, bali pia kama nyenzo ya kuelimisha na kuhamasisha wananchi kulinda mazingira.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa