Mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Mussa Kilakala ameongoza Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru leo Aprili 16,2024 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Muheza.
Mwenge wa Uhuru umepokelewa kwa kishindo na wananchi mbalimbali ambao wamejitokeza huku wakiimba nyimbo mbalimbali.
Mwenge wa uhuru ukiwa Pangani utakagua, utaweka mawe ya Msingi pamoja na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Miongoni mwa miradi itakayokaguliwa na kutembelewa na Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2024 ni pamoja na-"
Kikundi cha Kazi Mkazo, Ujenzi wa jengo la Pangani Fm Radio (UZIKWASA) wenye gharama ya Shilingi milioni 777, mradi wa ujenzi wa Madarasa 4 na Matundu 7 ya Vyoo ya Kidato cha 5 & 6 Shule ya Sekondari Funguni ambapo jumla ya Shilingi milioni 119 zimetumika.
Aidha Mwenge wa Uhuru pia utatembelea mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami mita 480, PANGADECO 11, pamoja na Ukarabati wa Hospitali ya Wilaya ya Pangani ambapo jumla ya Shilingi Milioni 900 zimetolewa na Serikali.
#Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu".#
#karibuMwengewaUhuru
#karibuPangani.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa