Mafunzo ya walimu mahiri wa somo la hisabati yenye lengo la kuboresha ujuzi wa walimu wa shule za msingi katika kufundisha hisabati yameendelea kutolewa leo tarehe 4 Februari 2025 katika ukumbi wa walimu TRC
Mafunzo hayo yamefunguliwa rasmi leo, tarehe 4 Februari 2025, na yanaendeshwa na mratibu wa mradi wa Shule Bora, Joseph Kyara, pamoja na wakufunzi kutoka Chuo cha Walimu Mandaka, kilichopo Mkoa wa Moshi, na Chuo cha Ualimu Korongwe.
Kwa kushirikiana na mradi wa Shule Bora, mafunzo haya yamekusudia kuwapa walimu mbinu bora za kufundisha, kuongeza ufanisi wao katika kufundisha, na kwa hivyo kuchangia katika ufaulu wa wanafunzi na kuongeza uwandikishaji wa wanafunzi shuleni.
Mafunzo haya yanatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika somo la hisabati katika shule za msingi na yatahitimishwa tarehe 7 Februari 2025.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa