Ikiwa leo ni kilele cha siku ya wazee Duniani Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Pangani sambamba na Ofisi ya Mbunge na Halmashauri kwa ujumla imefanyika Kampeni ya “NASHUKURU MZEE” ambayo imeacha alama kubwa na kuandika historia katika wilaya hii kwa kufanikisha yote yaliopangwa kufanyika ikihusisha Neno la kuwashukuru kwa kazi nzito waliofanya hadi sasa kuijenga Pangani na taifa letu kwa ujumla.
Kuwapa zawadi ya uhakika ambayo ni sekta ya Afya kama jambo muhimu zaidi kwao nyakati hizi ikiwa ni kuhakikisha wazee wote ndani ya siku hii wanapata vitambulisho vyao vya matibabu bure kama inavoelekeza sera ya wazee.
Moja ya mzee aliehudhuria siku ya wazee duniani akifanyiwa uchunguzi wa afya yake na wataalamu wa Afya kutoka Halmshauri
Matibabu,upasuaji, vipimo na matibabu bure maalum toka kwa wataalam ndani na nje ya Pangani kwa wiki hii hadi kilele,Vipimo vya macho na wataopatikana na tatizo kupatiwa miwani,Zoezi la uchangiaji damu.
Sambamba na zawadi hii ya kiafya pia ofisi ya mkuu wa wilaya ikishirikiana na Halmashauri imefanikiwa Kuwajengea uwezo na kuwapa tumaini jipya na mikakati sambamba na kusikilizaa changamoto zao.
wazee wa Pangani mjini waliohudhuria maadhimisho ya siku ya mzee duniani
Mwisho kushirikia pamoja nao chakula cha mchana Nyumbani kwa Mkuu wa Wilaya
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa