Vijana Pangani Watoa Shukrani kwa Serikali kwa Mikopo ya 10%

Vijana wilayani Pangani wameishukuru Serikali kwa kuwawezesha kupata mkopo wa asilimia 10 kupitia Halmashauri, wakisema umechangia kuwainua kiuchumi na kuongeza ajira.

Akizungumza leo 24 Novemba 2025 wakati wa ziara ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi, Mwenyekiti wa Kikundi cha Vijana wa Bodaboda Stendi ya Pangani Bw. Alhaji Kidau alisema:

“Tunashukuru Serikali kwa kutupatia mikopo kwa awamu mbili. Fedha hizi zimeleta mabadiliko makubwa kwenye maisha yetu na kutuongezea fursa za maendeleo.”. Alisema.
Kwa upande wake kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga mhe Sebabili amewapongeza Vijana hao kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya.
Aidha Vijana wa kikundi hicho wameahidi kuendelea kuitumia vizuri mikopo hiyo ili kuboresha kipato na kujenga uchumi wa jamii yao.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa