Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Ayubu Sebabili, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza, leo tarehe 24 Novemba 2025 amefanya ziara ya kikazi Wilayani Pangani kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, ikiwa na lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi.

Katika ziara hiyo, Mhe. Sebabili alipokea maoni, changamoto na mapendekezo kutoka kwa wakazi wa maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Pangani.
Aidha, aliwaagiza watendaji wa Serikali kuhakikisha kwamba kero zinazobainishwa zinashughulikiwa kwa haraka, kwa ufanisi na kwa kuzingatia maslahi ya wananchi.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Wilaya ya Pangani, Bi. Ester Zulu Gama, alisema kuwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025 jumla ya shilingi milioni 300 zimetolewa kwa vikundi mbalimbali vya vijana wilayani humo, na Halmashauri inaendelea kutenga fedha kwa ajili ya mikopo hiyo ili kuongeza fursa za kiuchumi kwa vijana.

Aidha, Mhe. Sebabili ameipongeza Halmashauri ya Pangani pamoja na wananchi kwa kuendelea kulinda amani na mshikamano, akisisitiza kuwa amani ndiyo msingi wa maendeleo, ustawi wa jamii na utekelezaji wa mipango ya Serikali.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa