Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mhe. Gift Isaya Msuya, ameongoza kikao cha tathmini ya utekelezaji wa afua za lishe kwa robo ya nne, mwaka wa fedha 2024/2025, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya zamani, leo tarehe 03 Oktoba 2025.

Aidha kikao hicho kimehusisha Wakuu wa Idara na Vitengo, Wataalamu wa Lishe,Maafisa Tarafa pamoja na
Watendaji Kata.

Lengo kuu la kikao hicho ni kujadili hatua zilizopigwa katika kupunguza changamoto za lishe wilayani Pangani na kuweka mikakati mipya ya kuboresha afya na ustawi wa wananchi.
Mhe . Gift amesisitiza umuhimu wa kila Shule kutoa huduma ya chakula kwa Wanafunzi ili kuinua kiwango chao cha ufaulu.

Hali ya Lishe katika Wilaya ya Pangani kwa ujumla iko vizuri na afua mbalimbali za lishe zinaendelea kutekelezwa.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa