Wahudumu wa afya ngazi ya Jamii Wilayani Pangani leo tarehe 21 Februari 2025, wamepatiwa vitendea kazi mbalimbali zikiwemo baiskeli zilizotolewa na Buffalo Bicycles pamoja na vifaa tiba zikiwemo sare, pamoja na vipimo vilivyotolewa na Shirika la Amref kupitia mradi wa Afya Himilivu , watakavyovitumia kuwafikia wananchi katika maeneo yao wakati wa kuwapatia huduma.
Akiongea mala baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Bw. Charles Edward Fussi, ameshukuru wafadhili na kuwaasa wahudumu wa afya kutumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyopangwa ili kuwasaidia wananchi.
Pia, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipa kipaumbele sekta ya afya na kuwapongeza wafadhili kwa mchango wao.
Kwa upande wake ndugu Bahati Rubeni Mwailafu kutoka Wizara ya Afya amempongeza Mkurugenzi Mtendaji kwa ushirikiano wake na kusisitiza kuwa juhudi hizi ni sehemu ya mpango wa Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan wa kuboresha huduma za afya katika jamii.
Hafla hiyo ya ugawaji wa vifaa inaonesha mwitikio wa serikali na washirika wake katika kuhakikisha kuwa huduma za afya zinawafikia wananchi, hasa katika maeneo yanayohitaji zaidi. Hii ni mfano wa jinsi ushirikiano kati ya serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, na wafadhili unaweza kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya afya.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa