Pangani _ Tanga.
"Tuzingatie Lishe Bora kulinda Afya zetu".
Kauli hiyo imebainishwa na Afisa Lishe Wilaya ndg Daud Mwakabanje mapema leo Septemba 25,2024 wakati wa muendelezo wa kampeni ya "Utumishi ni dili, zingatia Unachokula".
Kampeni hiyo ilioandaliwa na idara ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, imeendelea kuyafikia makundi mbalimbali, lengo ni kupima na kujua hali ya Afya na Lishe.
Aidha kampeni hii inahusisha zoezi la upimaji wa Hali ya Lishe pamoja na kupewa Elimu na unasihi wa kitaalamu ili kupunguza magonjwa yasiyoambukiza.
Askari wa Jeshi la Magereza Wilayani Pangani ni miongoni mwa kundi muhimu lililojitokeza kwa wingi kupima hali ya Lishe ( BMI Assessment), ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kampeni hiyo na wametoa wito kwa jamii kujua hali ya afya zao.
Ikumbukwe kuwa zoezi hili lina lengo la kuzifikia taasisi zote za Serikali zilizopo Wilayani Pangani pamoja na wananchi wote kwa ujumla.
#lisheboranimtaji.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa