Tanga -Pangani.
Leo Tarehe 10.12.2024 Askari wa kike wa dawati la jinsia na watoto wakishirikiana na kikosi Cha TPF -NET Mkoa wa Tanga, wametembelea hospitali ya Wilaya ya Pangani na kugawa baadhi ya vifaa Kwa wagonjwa ikiwa ni kuadhimisha kilele Cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Nae Mratibu Muandamizi wa Polisi ambaye pia ni mwenyekiti wa TPF-NET Mkoa wa Tanga (SSP), Hadija .A.Sokolo amesema kuwa
"Leo tumeamua kutembelea wagonjwa katika Hospitali hii Pangani kwa lengo la kuonyesha Jamii kuwa tupo nao karibu katika kukemea masuala ya ukatili wa kijinsia ,"Alisema kamanda Sokolo .
Akizungumza mala baada ya kupokea vifaa hivyo kwa niaba ya uwongozi wa Hospitali hiyo, kaimu Mganga Mkuu ndg, Nikson amesema kuwa
"Tunawashukuru kwa msaada wa vitu hivi na kuikumbuka jamii, vitu hivi vitawarejeshea na kuwaongezea tabasamu wagonjwa hawa ".Alisema.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa