M
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Pangani leo tarehe 16 Mei 2024 limekutana na kufanya Kikao chake cha kwanza katika mfululizo wa vikao viwili vya Baraza la Madiwani la Halmashauri, vikao ambavyo vimepangwa kufanya tarehe 16-17 Mei 2024.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri ambapo Taarifa za Utendaji kazi kwenye ngazi ya Kata kwa robo ya Tatu mwaka 2023/2024 ziliwasilishwa.
Akipokea taarifa hizo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Mhe. Akida Bahorera aliwapongeza na kuwashukuru Waheshimiwa Madiwani wa Kata zote 14 kwa kazi nzuri walizozifanya katika kipindi cha robo ya Tatu kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2023/2024, ikiwa ni pamoja na kusimamia kwa ukaribu miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.
Taarifa za Utendaji kazi kwenye ngazi ya kata zilizowasilishwa ni pamoja na kata ya Mikinguni, Kipumbwi,Mkwaja,Tungamaa,Mwera,Bweni,Pangani Magharibi, Pangani Mashariki, Kimang'a Madanga, Bushiri, Masaika , Mkalamo na Ubangaa, ambapo waheshimiwa walitoa michango yao mbalimbali juu ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa