BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA MPANGO NA BAJETI YA SHILINGI BILIONI 19.5
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Mheshimiwa Akida Bahorera Leo tarehe 05 Machi 2024 ameongoza Mkutano wa Baraza la Madiwani, katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, kujadili na kupitisha rasimu ya Mpango na Bajeti ya mwaka 2024/2025.
Baraza hilo limeridhia kupitisha rasimu ya Mpango na Bajeti ya Shilingi Bilioni 19.5 kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Aidha Waheshimiwa Madiwani wameonyesha maono chanya katika maandalizi ya mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 ikiwemo Baraza la wafanyakazi, kamati ya ukimwi, kamati ya elimu, kamati ya uchumi, ujenzi na mazingira, kamati ya fedha, Utawala na mipango.
Hata hivyo katika Baraza hilo la kupitisha rasimu ya bajeti Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Pangani Ndugu Juma Mbwela amewapongeza Waheshimiwa Madiwani wa kata zote 14, kwa kuendelea kuwa wafuatiliaji wa karibu miradi ya maendeleo na michango yao katika kuendeleza Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Kwa upande wa TARURA walieleza kuwa Wilaya ya Pangani inapendekeza kutumia jumla ya Shilingi Bilioni 2.7 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya barabara.
Mhe Akida Bahorera amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha za miradi ya Maendeleo Wilayani Pangani,pamoja na mhe Jumaa Aweso mbunge wa Pangani kwa kuisemea vizuri Pangani, Mkuu wa Wilaya mhe Zainab Abdallah, pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo.
#miakamitatuyamama
#kaziiendelee.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa