Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, umeketi leo Aprili 30,2025, katika ukumbi wa Halmashauri ya zamani ikiwa ni hitimisho la Robo ya Tatu kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Akida Bahorera, amesema kuwa Mkutano huo umelenga kuwasilisha na kujadili taarifa za Utendaji kazi kwa kipindi cha robo ya tatu, hivyo ni kikao muhimu kwa maendeleo ya Halmashauri yetu.
" Wilaya yetu ni miongoni mwa Wilaya zilizotulia katika Mkoa wetu wa Tanga, na sote tunaona maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya pamoja na miundombinu ya barabara inaendelea kuboreshwa". Alisisitiza.
Sambamba na hayo taasisi mbalimbalia za Serikali ikiwepo TARURA, TANESCO na TANGAUWASA, RUWASA, zimewasilisha taarifa zao katika mkutano huo.
Hata hivyo taarifa mbalimbali za kamati za Kudumu ziliwasilishwa katika mkutano huo ikiwemo taarifa ya kamati ya fedha, mipango na uongozi, taarifa ya kamati ya elimu na afya, taarifa ya kamati ya uchumi, ujenzi na mazingira pamoja na kamati ya kudhibiti ukimwi na kujadiliwa ikiwa ni utekelezaji wa Robo ya tatu kuanzia mwezi Januari hadi Machi, kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa