Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Ndugu Agape Fue, ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi, amefungua mkutano wa baraza hilo la kujadili na kupitisha rasimu ya mpango na bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani kwa mwaka wa fedha 2025/2026, leo tarehe 04 Machi 2025, katika Ukumbi wa Zamani wa Halmashauri.
Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Ndugu Simeon Vedastus aliwasilisha rasimu ya mpango na bajeti ya Halmashauri kwa wajumbe wa baraza la wafanyakazi ili iweze kujadiliwa na kupitishwa katika baraza hilo kabla ya kuanza utekelezaji wake.
" Pamoja na maelekezo mbalimbali tulioelekezwa na Serikali lakini yapo mambo mbalimbali tuliyoyafanyia kazi ikiwemo posho za uhamisho kwa walimu wa shule za Msingi na Sekondari, madeni ya watumishi, madeni ya wazabuni, fedha za posho ya watendaji wa kata,fedha za madaraka kwa wakuu wa shule, waratibu Elimu kata na walimu wakuu, posho ya wito wa kuwepo kazini pamoja na uendeshaji wa ofisi za kata, hivyo Halmashauri yetu inatarajia kukusanya na kutumia jumla ya Shilingi bilioni 23.9 kwa Mwaka wa fedha 2025/2026 ". Alifafanua.
Wajumbe walipata nafasi ya kuchangia na kutoa mapendekezo mbalimbali ambayo kwa pamoja yalifanyiwa kazi na kuboreshwa.
Baraza la wafanyakazi lilipitisha rasimu ya mpango na bajeti, ambapo kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Halmashauri ya Wilaya ya Pangani inatarajia kukusanya na kutumia kiasi cha Tshs Billioni 23.9 ikijumuisha fedha za mapato ya ndani, miradi ya maendeleo, mishahara matumizi mengineyo pamoja na ruzuku kutoka Serikali kuu.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa