Biashara ya Kaboni (Hewa Ukaa) yawavutia Waheshimiwa Madiwani, Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Timu ya Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ikijumuisha Madiwani pamoja na Wataalamu wamefanya ziara Mkoani Katavi Wilayani Tanganyika kwa lengo la kujifunza namna ambavyo Halmashauri hiyo imetekeleza na kunufaika na Biashara ya hewa ukaa.
Ziara hiyo imefanyika leo tarehe 20 Desemba, 2024.
Awali akiwasilisha mada ya mradi wa hewa ya kaboni (ukaa ), Mkuu wa Kitengo cha Maliasili Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Bw.Bruno Mwaisaka amewaambia Madiwani na Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, kuwa ili waweze kunufaika na Biashara ya Hewa ya Kaboni ni muhimu kuwepo kwa manufaa kwa jamii inayolinda misitu hiyo pamoja na ongezeko la thamani kwa msitu hio.
Ameongeza kuwa ni muhimu kuzingatia muongozo wa Kitaifa wa uanzishaji wa Biashara hiyo ya hewa ya kaboni pia Biashara ya kaboni ina mfumo wake kupitia shirika la Verra na ina masoko aina mbili ambalo ni la hiari na soko la umoja wa Mataifa. Alisema.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani mhe Akida Bahorera amesema kuwa Wilaya ya Pangani tuna misitu mizuri sana na elimu hii tulioipata leo itasaidia na sisi kuwekeza zaidi katika biasha hii yenye kuongeza pato kwa Halmashauri.
Hata hivyo mhe Haji Haji diwani wa kata ya Madanga Wilayani Pangani ameonyesha kufurahishwa na ziara hiyo na kusema kuwa ziara hii imetupa fursa ya kuelewa namna ambavyo wananchi watakavyo weza kunufaika kupitia Mradi wa Uvunaji wa Hewa Ukaa katika Misitu inayomilikiwa na Vijiji pamoja na Halmashauri.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa