Kamati za Usimamizi wa Mazingira ya Baharini (BMU) kutoka Wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi, imefanya ziara ya mafunzo leo tarehe 23 Juni 2025, katika Halmashauri ya Wilaya ya Pangani kwa lengo la kujifunza mbinu bora za ukusanyaji wa mapato yatokanayo na rasilimali za bahari.
Ziara hiyo iliyowakutanisha wajumbe kutoka BMU kutoka Kilwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa na viongozi wa idara husika Pangani, imelenga kubadilishana uzoefu na kujifunza mifumo ya kiufanisi inayotumika Pangani katika kusimamia rasilimali za baharini na kuhakikisha mapato yanaongezeka kwa ajili ya maendeleo ya jamii husika.
Ziara hiyo imefungua fursa ya ushirikiano kati ya wilaya hizo mbili katika kusimamia mazingira ya pwani na kuhakikisha ustawi wa wakazi wanaotegemea shughuli za baharini kwa maisha yao ya kila siku.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa