Shule ya Msingi Bushiri ni kati ya Shule kongwe iliopo kata ya Bushiri Wilayani Pangani.
Kutokana na miundombinu chakavu ya shule hii kongwe ya Bushiri, Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassani,ilitenga Fedha shilingi milion 446.5, kwaajili ya ujenzi wa Shule Mpya, Matundu ya Vyoo pamoja na Nyumba ya Mwalimu ili kuleta mazingira rafiki ya kujifunzia.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Bwan. Isaya M Mbenje, ametoa shukrani zake kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mala baada ya kukagua maendeleo ya Mradi huo.
"Napenda kutanguliza shukrani zangu kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha za ujenzi wa Shule ya Msingi Bushiri, Shule yetu likuwa katika hali mbaya,ikiwemo uchakavu uliopitiliza wa madarasa, hivyo tuliona ni vema kuomba fedha kwaajili ya ujenzi wa shule hii mpya yenye mazingira rafiki".
Bwan. Mbenje ameongeza kuwa ujenzi umekamilika kwa asilimia 95% , hatua iliyopo ni kupaka rangi na kufunga Alminium na Shata na tayari tumeshapeleka jumla ya madawati 100.
Hata hivyo Mbenje ametoa shukrani nyingi kwa wananchi wa Bushiri kwa kufanikisha utekelezaji wa ilani ya CCM na usimamizi mzuri wa Mhe. Zainab Abdallah, Mkuu wa Wilaya ya Pangani na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Waziri Kindamba kwa maelekezo bora ya kufanikisha Mradi huu.
Hadi sasa ujenzi wa Shule hii upo katika hatua za mwisho za ukamilishaji.
#panganimpya
#elimukwanza
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa