Pangani_ Tanga.
Katibu Tawala Wilaya ya Pangani Bi Ester Gama kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Gift Isaya Msuya leo Agosti 19, 2024 ameongoza kikao cha kamati ya lishe kujadili tathimini ya Mkataba wa Lishe Robo ya Nne Aprili hadi Juni kwa mwaka wa fedha 2023/2024, katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya zamani.
Bi Ester Gama amesisitiza kuwa agenda ya lishe iwe endelevu na kuwataka wataalam wa Lishe na watendaji kata wote na kijiji kuhakikisha elimu kuhusu lishe inaendelea kutolewa kwa kila mhusika na kusimama imara kuhakikisha suala la lishe linatekelezwa kwa ubora katika Wilaya ya Pangani.
Akiwasilisha taarifa ya Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Afisa Lishe Wilaya bw Daud Mwakabanje amesema kuwa
" katika robo ya nne kitengo cha lishe kimefanya tathmini ya hali ya lishe kwa wananchi kwa kutumia kipimo cha uwiano wa uzito kwa urefu(BMI), kufanya usimamizi shirikishi shuleni, kufanya Maadhimisho ya Siku ya afya na lishe katika vijiji(SALiKi) pamoja na kushiriki katika utoaji wa huduma wa afya mseto( afya gulio), in pamoja na kutoa mafunzo ya mguso katika Wilaya ya Pangani". Alisema.
Kwa upande wake mhe Akida Boramimi Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu na Afya amesisitiza kuwa usimamizi imala kwa watendaji wote ili kutekeleza kwa vitendo afua za lishe katika jamii zetu.
Taarifa zingine zilizojadiliwa ni kadi alama kwa ngazi ya kata na Halmashauri pamoja na viashiria mbalimbali vya lishe ambavyo vipo kwenye ilani ya chama Tawala ambapo afisa lishe amebainisha kuwa tuko vizuri kwa asilimia zote 100, na kuendelea kutoa elimu katika jamii.
Utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi shuleni ni muhimu kwa afya bora, mahudhurio mazuri, kuongeza ufaulu pamoja na kupunguza utoro.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa