Leo tarehe 16 Februari 2024 Katibu Tawala Wilaya ya Pangani Bi. Ester Gama amefungua na kuongoza kikao cha tathmini ya mkataba wa lishe ngazi ya kata kwa robo ya Pili kuanzia mwezi Oktoba -Disemba 2023/2024 kilichofanyika katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Katika ufunguzi huo katibu Tawala amesema kuwa kikao hiki ni kikao nyeti na jambo la Lishe ni Jambo la Kitaifa, na sote tumekuwa mashahidi kumuona Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa mstari wa mbele kuhakikisha Afya za Watoto zinaimarika.
Akisoma taarifa ya Lishe Afisa Lishe Wilaya ya Pangani Bw. Daud Mwakabanje amesema agenda ya Lishe Wilayani iwe ni ya lazima.
" Ni muhimu kutoka elimu kwa wananchi, katika kutekeleza Afua za Lishe kwa vitendo tumefanya kampeni ya umezeshaji wa matone ya Vitamini A, pamoja na kufanya maadhimisho ya ya Siku ya Lishe na Afya kwa kila kijiji na tumewafikia wananchi 7697 kwa robo hii ya Pili".
Vilevile ameongeza kuwa kuna changamoto kwa wakina Mama Wajawazito kutohudhuria Kliniki kwa wakati na pia kutotumia kwa wingi mbogamboga, lakini sisi kama Wilaya tumeendelea kutoa elimu kupitia vyombo vyetu vya habari ikiwemo kurasa zetu rasmi za Halmashauri pamoja na radio Pangani ili kuendelea kuwajengea uelewa zaidi Wananchi juu ya masuala mtambuka ya Lishe.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ndg Ramadhan Hussein amesisitiza kuwa usimamizi shirikishi unaendelea na Wataalam wanatekeleza usimamizi huo ili Elimu ya Lishe iweze kumfikia kila mmoja wetu.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa