Rai hiyo imetolewa mapema leo tarehe 31 Januari 2025 na Katibu Tawala Wilaya ya Pangani Bi Ester Gama wakati wa mkutano wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani lililoketi kupokea na kujadili taarifa za kamati mbalimbali kwa kipindi cha robo ya pili kuanzia mwezi Oktoba hadi Disemba 2024/ 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya zamani.
" Ukusanyaji wa mapato si jambo la Wataalamu pekee bali ni jambo letu sote, hivyo tujikite kwa pamoja kuhakikisha tunakusanya kwa bidii mapato ili Halmashauri yetu isonge mbele". Alisema.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri hiyo mhe Akida Bahorera amesema kuwa timu yake ya waheshimiwa madiwani ipo tayari na inashirikiana vema kuhakikisha mapato yanakusanywa.
Sambamba na hilo Baraza la Waheshimiwa Madiwani limeipongeza ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Pangani pamoja na Mkurugenzi Mtendaji kwa kuendelea kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa