DC AHITIMISHA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA
Mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Zainab Abdallah Jumatatu Novemba 13,2023, ameitimisha Mafunzo ya Jeshi la Akiba (Mgambo) kwenye hafla iliyofanyika Kata ya Kipumbwi Halmashauri ya Pangani.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Mkuu wa wilaya ya Pangani amewaasa vijana wote waliomaliza mafunzo hayo, kuwa watii na wazalendo kwa Taifa lao na kuhakikisha wanatumia maarifa waliyoyapata kuendeleza amani na utulivu katika nchi hii.
Aidha amewakumbusha utii kwa viongozi wote na kwa kuwa Mhe. Rais Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka mfumo mzuri wa majeshi ya Ulinzi na wao kwa sasa ni sehemu ya Ulinzi wa Taifa.
"Tumieni mafunzo haya kulitumika Taifa na zaidi katika kulinda raia na mali zao na siyo kuvunja sheria za nchi, kwa serikali imewaamini na kuwapa mbinu za ulinzi na usalama wa raia, hiyo jukumu lenu kubwa ni kuwatumikia wananchi". Amesema Mkuu huyo wa Wilaya
Wakisoma Risala yao kwa mgeni sasmi, vijana 85 wameiomba serikali kuendelea kutoa fursa ya mafunzo hayo mara kwa mara ili kukuza na kuendeleza maarifa na ujuzi katika kazi.
Katika sherehe hizo mkuu wa wilaya aliambatana nawajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, viongozi wa halmashauri ya Pangani , viongozi wa Chama, pamoja na wananchi.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa