DC ASHIRIKI HAFLA YA KUFUNGA MAFUNZO YA UTALII KWA VIJANA WA PANGANI.
Mkuu wa wilaya ya Pangani Mh. Zainab Abdallah, Septemba 11, 2023, ameshiriki hafla ya ufungaji wa Mafunzo ya Utalii kwa Vijana wa Pangani.
Hafla hio ya ufungaji wa mafunzo ya Siku tano (5) ya Utalii yaliotelewa na wakufunzi kutoka Chuo cha Taifa cha Utalii, ambapo mada mbalimbali kuhusu utalii zilifundishwa na njia bora za kutangaza na kutunza vivutio vilivyopo Pangani na faida zake.
Ufungaji wa Mafunzo hayo yamehudhuriwa na Mkuu wa Chuo cha Utalii Dkt Florian Mtey, Makamu mkuu wa chuo Jesca Willium, katibu tawala Ester Gama, Diwani wa kata ya Kimang'a mhe Mwandalo Salim, Pamoja na Makamu mkuu wa chuo cha Utalii.
Mhe Zainab ameishukuru menejiment nzima ya chuo cha utalii, na Serikali ya Pangani pamoja na wadau wote walioshiriki mafunzo haya.
Hata hivyo mhe Zainab Abdallah amesema kuwa ameunga mkono juhudi za Serikali za kutangaza Utalii kwa vitendo, na tayari amerekodi filamu ya vivutio vya utalii katika Wilaya ya Pangani.
Hata hivyo Mbunge wa Jimbo la Pangani mhe Jumaa Aweso amepongeza juhudi hizo na kutoa fursa kwa vijana kumi kuwasimamia katika masomo yao ya utalii kwa wale ambao watapata sifa za kwenda kujiunga na Chuo hiko, na kuahidi kuendeleza mafunzo hayo angalau kila mwaka ili kutoa fursa kwa vijana wengi zaidi.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Utalii dkt Florian Mtey, amemshukuru mkuu wa Wilaya ya Pangani kwa kuendelea kuipigania Pangani,na kuwa mzalendo wa kweli na kuongeza kuwa viongozi wa Pangani wanafanya kazi nzuri na Wilaya inawaka kwa maendeleo.
Hata hivyo ufungaji wa mafunzo hayo ulihusisha ugawaji wa Vyeti kwa wanafunzi walioshiriki pamoja na kupewa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi zaidi ya 20, katika Chuo cha Taifa cha Utalii .
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa