Pangani_ Tanga
"Hata vitabu vyetu vya dini, vimeeleza wazi juu ya umuhimu wa elimu, tukiendelea kuziishi falsafa za Baba wa Taifa mwalimu Julius K Nyerere,alisema kuwa elimu ndo chanzo cha ukombozi wa kupata jamii mpya na endelevu".
Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Zainab Abdallah, Jumanne, Oktoba 17,2023, wakati wa ufunguzi wa mdahalo maalumu na kutoa somo kwaajili ya kujadili Mradi wa Uwajibikaji Jamii na Mamlaka Zinazohusika katika kuboresha Elimu ulioandaliwa na shirika la TREE OF HOPE
Mdahalo huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa zamani wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani,ambapo mambo mbalimbali kuhusu elimu yalipata nafasi ya kujadiliwa kwa maslahi ya kukuza elimu katika Wilaya ya Pangani.
"Ni wakati sahihi wakuendelea kuipa thamani elimu katika Wilaya yetu ya Pangani, Sote ni mashahidi Serikali yetu chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan, imeendelea kutuletea miradi mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa madarasa bora ya kusomea, jamii inayo nafasi ya kuendelea kuwa sehemu ya ukuzaji wa elimu".
DC amewataka wazazi pamoja na wanafunzi kuipa nafasi ya kwanza elimu kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Goodluck Mariro, Mratibu wa Mradi katika shirika la TREE OF HOPE, amebainisha mafanikio ya uwekezaji katika elimu ikiwa ni pamoja na kuongeza ufanisi katika masuala yote ya kiuchumi pamoja na kupata jamii yenye fikra za ukombozi.
#panganimpya
#elimubora
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa