DC AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA 62 YA UHURU.
Mheshimiwa Zainab Abdallah Issa Mkuu wa Wilaya ya Pangani amewataka wananchi wa Pangani kupanda miti na kutoitelekeza miti hiyo iliyopandwa.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo leo tarehe 8 Desemba 2023 wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti kuelekea maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara.
Hata hivyo ametoa wito kwa jamii kuendeleza utamaduni wa kupanda miti na kueleza kuwa ni muhimu kwani ni zoezi la kuhifadhi Mazingira.
Miti hiyo imefanikiwa kupandwa kwenye maeneo ya viwanja vya Bomani, pamoja na maeneo ya Ferry ambapo miti aina ya mikoko imepandwa.
Aidha ameeleza umuhimu wa kupanda miti ikiwa ni pamoja na kutunza mazingira na kupata mbao, matunda na kivuli.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa