Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mhe. Zainab Abdallah amekabidhi rasmi ofisi kwa Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mhe. Mussa Kilakala leo Machi 18, 2024.
Akizungumza mala baada ya makabidhiano hayo DC Kilakala amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kumteua awatumikie wananchi wa Pangani na kuwaomba wananchi wote kutoa ushirikiano katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya kuijenga Pangani.
"Kipekee nimekuja Pangani kufanya kazi, kushirikiana na Wananchi wote,taasisi zote zilizopo Pangani,hivyo basi tushikamane kuijenga Pangani".
Aidha Dc Zainab Abdallah amewashukuru wananchi wote wa Pangani,Watumishi kwa ushirikiano waliomuonyesha kwa kipindi chote alicho watumikia.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa