Mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Mussa Kilakala leo tarehe 18 Mei, 2024 ameongoza kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri.
Akiwasilisha taarifa ya hali ya Lishe kwa kipindi cha robo ya Tatu, Afisa Lishe Wilaya ndg Daudi Mwakabanje amesema kuwa,
" Halmashauri ya Wilaya ya Pangani kupitia Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe imekua ikitekeleza afua mbalimbali za Lishe kwa kufuata mwongozo wa Taifa wa Lishe na kutoa Elimu na unasihi wa Lishe, kushiriki katika ufunguzi wa program jumuishi ya Taifa (PJT_MMMAM) katika ngazi ya Halmashauri, kufanya Maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe katika vijiji 33, kufanya usimamizi shirikishi katika vituo vya kutolea huduma za Afya pamoja na kufanya vikao".Alisema.
Sambamba na hilo Afisa Lishe amebainisha kuwa jumla ya wateja 264 waliohudhuria kliniki ya Baba ,Mama na mtoto katika hospitali ya Wilaya, vituo vya Afya na Zahanati wamepatiwa elimu.
Amebainisha kuwa katika kipindi cha robo ya Tatu, jumla ya watoto 2 waliogundulika na utapiamlo mkali wamepatiwa matibabu.
Sanjari na hayo, mhe Mussa Kilakala amewataka watendaji kata,Maafisa Tarafa pamoja na Maafisa kilimo, kuendelea na uhamasishaji wa utoaji wa chakula shuleni na kubainisha faida za wanafunzi kupata chakula shuleni na jinsi itakavyosaidia kupunguza utoro.
Aidha Halmashauri kupitia Sehemu ya huduma za lishe kwa kushirikiana na kitengo cha mawasilian o ya Serikali kimeendelea kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kufikisha Elimu ya Lishe kwa wananchi.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa