Mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Mussa Kilakala leo Aprili 24, 2024 ameongoza zoezi la kufanya usafi wa mazingira na upandaji miti.
Zoezi hilo la usafi limefanyika maeneo ya Soko Kuu la Pangani, ambapo limetambatana na upandaji wa miti katika Shule ya Sekondari Funguni, ikiwa ni maandalizi ya maadhimisho ya miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanayotarajiwa kufanyika Aprili 26 mwaka huu.
Katika zoezi hilo, miti 500 imepandwa katika eneo la Shule ya Sekondari Funguni iliyopo Kata ya Pangani Magharibi.
Akizungumza mala baada ya zoezi hilo Mhe Mussa Kilakala amesema
"kuelekea miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wilaya ya Pangani imeshiriki zoezi la kufanya usafi na kupanda miti na uhifadhi wa mazingira na kuhimiza juu ya utunzaji wa mazingira kwa kuendelea kupanda miti katika maeneo mbalimbali, hivyo tuendelee kulinda maeneo haya kwa kufanya usafi, kila mwananchi auchukie uchafu kwenye maeneo yake ". Alisema
Aidha kwa upande wake Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ndg Daud Mlahagwa amesema kuwa :-
"Zoezi la usafi wa mazingira na upandaji wa miti linapaswa kuwa endelevu kwa maeneo yetu, ikiwa ni sehemu ya utunzaji wa mazingira". Alisema.
Katika zoezi hilo wananchi mbalimbali,pamoja na watumishi wa Serikali wamejitokeza na kushiriki ufanyaji wa usafi huo na upandaji miti ikiwa ni sehemy ya utunzaji wa mazingira.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa