Pangani, Tanga.
Mkuu wa Wilaya ya Pangani, mhe Mussa Kilakala tarehe 1.08.2024 ametembelea mradi wa machinjio na kuhakikisha unakamilika kwa wakati ili wananchi waanze kunufaika nao.
Akiwa katika ziara hiyo Mheshimiwa KILAKALA alibaini changamoto ya upatikanaji wa umeme na maji na kumuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha anasimamia kukamilika kwa miundo mbinu hiyo (maji na umeme) ndani ya machinjio hayo.
Sambamba na hilo amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ndugu Charles Edward Fussi kuhakikisha ukarabati wa mradi huu unafanyika kwa ubora na viwango ili machinjio hayo yawe ya kisasa na kuiingizia Serikali mapato.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa