Mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Gift Isaya Msuya Leo Tarehe 7 Februari,2025, amegawa vitendea kazi Komputa Mpakato (laptop 5) kwa Maafisa Tarafa wa Tarafa nne pamoja na Ofisi ya Katibu Tawala, kama ilivyoelekezwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa kazi na utoaji huduma na kuimarisha matumizi ya teknolojia kidijitali.
Hatua hii imechukuliwa kama sehemu ya juhudi za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuboresha utoaji huduma kwa Umma.
Na kurahisisha utendaji kwa watumishi kwa kuwa taarifa zote za Kiutumishi zinatolewa kidijitali.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa