Pangani_Tanga.
"Tunaomba mtusadie kufikisha Salamu zetu kwa Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kazi nzuri na kubwa anayoifanya hata katika kuiletea miradi mbalimbali ya maendeleo Wilaya yetu ya Pangani, likiwemo daraja la mto Pangani".
Hayo ameyasema Jumanne ,Oktoba 3, 2023, Mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe. Zainab Abdallah wakati wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji,lililofanyika katika ukumbi wa YMCA, Pangani, na kuhudhuliwa na Wageni mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara mhe Exaud Silaoneka Kigahe, ambae ndio mgeni rasmi wa Kongamano hili.
Aidha ameongeza kuwa hili ni Kongamano la ndani la Biashara na Uwekezaji lakini tarehe 7 tutakuwa na Kongamano kubwa jijini Dar es Salaam, hivyo tunawakaribusha sana.
DC, ametoa ombi la kuwa na bandari ya Mifugo kwasababu mifugo mingi inatokea katika ukanda wetu, kama kuna uwezekano wa kuwa na bandari maalumu hapa Pangani, kwani tunaweza kuwa na bandari yetu na hii itaongeza mapato ya Serikali na kuongeza pato kwa wananchi wetu, na tayari tuna muwekezaji ambae yupo tayari kuwekeza hapa Pangani.
Aidha ameiomba Wizara ya Biashara na Uwekezaji , kushuka chini mpka kwenye ngazi za Wilaya, na tuko tayari hata kutoa ofisi kwaajili ya watumishi wa Blera na Sido kuja kuanza kazi.
Mwisho ametoa wito kwa Wawekezaji kuja kuwekeza katika Wilaya ya Pangani na Mazingira ni salama kwa wawekezaji.
"Ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa Wilaya yetu hii ya Pangani imeshafunguka kibiashara, hivyo, ni wakati sahihi kwa wawekezaji kuja kuwekeza katika Wilaya hii kwani tunayo ardhi yenye rutuba na bora".
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Bw. Isaya M Mbenje, mapema leo Octoba 3,2023, Wakati wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji Pangani.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa