Mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Mussa Kilakala akitoa salamu za Serikali, mapema leo Mei, 17,2024 wakati wa mkutano wa baraza la Madiwani katika kipindi cha robo ya Tatu kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2023/2024, amesisitiza matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Sambamba na hilo mhe Mussa Kilakala amesema kuwa mbunge wa jimbo la Pangani ambaye pia ni Waziri wa maji mhe Jumaa Aweso alitamani kushiriki baraza hilo lakini kutokana na majukumu mengi ameomba kuwakilishwa na katibu wake.
Aidha mhe Mussa Kilakala ametoa salamu kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga cde Rajab Abdurrahman ambapo amesema kuwa yupo pamoja na wanapangani katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa ukubwa wake.
Mwisho ametoa salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe Samia Suluhu Hassan, ambapo amesema kuwa ni wakati sahihi wananchi kuunga mkono mpango wa nishati safi ya kupikia (gesi).
" Rais anahakikisha maeneo yetu ya vijijini gesi iwe inapatikana ili wananchi waweze kutumia nishati safi na salama ya kupikia" Alisema.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa