"Sekta ya utalii imekuwa sana na kuna wageni zaidi ya milioni tatu wanaotembelea vivutio vyetu vya utalii Tanzania, ni ombi langu tupate boti za kisasa zitakazo tumika kufanya shughuli za kusafirisha wageni kutoka Zanzibar na kuja Pangani".
Hayo yamesemwa leo Jumanne, Oktoba 10,2023, na Mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Zainab Abdallah katika Ziara ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar mhe Hemed Suleiman Abdullah, iliofanyika katika ukumbi wa YMCA ,Pangani.
Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar mhe Hemed S Abdulla, ameahidi kuwa suala hilo la Boti lipo katika mchakato na muda mfupi ujao litatatuliwa .
Hata hivyo, Makamu wa Rais wa Zanzibar,mhe Hemed Suleiman Abdulla, ameendelea kutoa wito kwa wanapangani kuendelea kushirikiana na viongozi mbalimbali ili kuleta maendeleo makubwa katika Wilaya hio.
#panganimpya
#hakunakilichosimama.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa