Mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Mussa Kilakala amezindua kampeni ya "Soma na Mti" ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali kuhakikisha kila Halmashauri inapanda miti isiyopungua 1,500,000 kila mwaka.
Hayo yamefanyika leo Aprili 11,2024 katika shule ya Msingi Funguni ambapo jumla ya miti 2500 imepandwa.
Aidha zoezi hilo limetekelezwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tree of Hope na imekabidhi miti mbalimbali ya mitunda na mikoko, ambapo jumla ya miti (2500), imetolewa ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali za upandaji miti.
"Tunashukuru kwa ushirikiano mzuri tunaopata Wilayani Pangani na tutaendelea kuungana na wanapangani katika kuikijanisha Pangani alisema".
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mhe Kilakala amesema kuwa lengo la Wilaya ni kupanda miti zaidi ya Milioni moja na laki Tano ,hivyo tunawashukuru sana na tutahakikisha Pangani yetu inakuwa ya kijani.
"Wote tunafahamu faida ya miti, tukipanda hii miti na kuitunza tutaleta mafanikio makubwa sana katika Wilaya yetu ya Pangani" tuitunze miti hii kwa vizazi vijavyo".
Ameendelea kuwataka wadau kuleta miti kwa wingi na kushiriki katika kupanda miti.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa