Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mhe. Zainab Abdallah na Mkurugenzi wa Taasisi ya Nasimama na Binti, Wema Isack Sepetu, wametembelea na kuzungumza na wanafunzi wa Shule za Sekondari Kipumbwi, Bushiri, Kimang'a na Mwera,zilipo wilayani Pangani.
Akiongea na wanafunzi wa shule hizo amewataka kuongeza bidii kwenye Elimu ili waweze kufanikiwa huku akitoa shukrani kwa Rais,Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha Pangani kwenye miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Shule.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Nasimama na Binti, Wema Isack Sepetu, amesema kuwa anamshukuru sana Mkuu wa Wilaya ya Pangani kwa kumpa mualiko wa kutembelea shule hizo,na ameahidi kuwa atawasaidia wanafunzi wakidato cha nne wa Shule ya Sekondari Kipumbwi, watakao pata daraja la kwanza kwenye mitihani yao na atawasimamia katika masomo yao mpaka watakapo maliza, sambamba na hilo Wema Sepetu, amegawa zawadi mbalimbali katika Shule hizo ikiwa ni pamoja na Jezi,daftari, pamoja na madawati 50 kwa shule zote alizotembelea pamoja na Kalamu ili kuwasaidia wanafunzi hao kusoma kwa bidii.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Mhe Akida Bahorera amepongeza juhudi za Mkuu wa Wilaya pamoja na Wasanii wote waliojitokeza kutembelea Shule hizo mbili kwani ujio wao umeleta chachu ya taaluma kwa Wanapangani na ametoa wito kwa Wanafunzi wa Mwera na Kipumbwi kuendelea kuongeza juhudi katika elimu.
Katika ziara hii DC ameambatana na Wasanii wengine ambao ni Maarifa,Mimah Pamoja na Ruby, kwaajili ya kuendelea kutoa Elimu kwa Wanafunzi juu ya masuala mbalimbali.
Ziara hii itahitimishwa Agosti 19, 2023 na itaambatana na uzinduzi wa kampeni ya NIACHE NISOME PANGANI INANITEGEMEA, na Mgeni Rasmi atakuwa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda.
#panganimpya
#niachenisome
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa