Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ndg Charles Edward Fussi, leo tarehe 3, Oktoba 2024, ameshiriki mafunzo maalumu ya Usimamizi na utoaji wa mikopo Kwa vikundi vya Wanawake Vijana na Watu wenye ulemavu, kwa Kamati za huduma za mikopo ngazi ya Kata.
Hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Zamani, mala baada ya kutangazwa kwa dirisha la maombi ya Mikopo hiyo kufunguliwa.
Aidha ndg Charles Edward Fussi amebainisha kuwa Jumla ya Shilingi Milioni 254.9 zimetengwa hivyo Vikundi venye sifa vijisajili na kuomba mikopo hiyo kwenye mfumo wa Wezesha portal.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bi Sekela Mwalukasa ameahidi kushirikiana na kamati za mikopo kusimamia kanuni na miongozo ya utoaji wa mikopo kwa vikundi hivyo.
" Mafunzo haya yanalenga kuwajengea uwezo kamati za huduma za mikopo ngazi ya Kata juu ya kanuni na miongozo ya utoaji na usimamizi wa mikopo ya vikundi vya Wanawake anawake Vijana na Watu wenye Ulemavu". Alifafanua".
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa