Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Bw. Isaya M Mbenje amekabidhi rasmi ofisi kwa Mkurugenzi Mtendaji Bw. Edward Charles Fussi.
Hayo yamefanyika leo Machi 27, 2024 katika ukumbi wa Halmashauri,Mkoma, na kuhudhuriwa na Mhe Akida Boramimi diwani wa kata ya Pangani Mashariki akimuwakilisha Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na wakuu wa idara na Vitengo.
Akizungumza mala baada ya makabidhiano hayo Bw Fussi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kumhamishia katika Wilaya ya Pangani awatumikie wananchi.
Aidha amewaomba watendaji, na wananchi wote wa Wilaya ya Pangani kutoa ushirikiano katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya kuijenga Pangani.
Mhe Boramimi ametumia wasaa wake kumshukuru Bw. Isaya M Mbenje kwa kuitumikia Pangani kwa kipindi chote alichohudumu na amemkaribisha Bw Edward Charles Fussi na kuahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwa maslahi ya kuijenga Pangani.
Kwa upande wake Bw Isaya M Mbenje amewashukuru waheshimiwa madiwani, watumishi na wananchi wote wa Wilaya ya Pangani kwa ushirikiano waliomuonyesha kwa kipindi chote alichowatumikia.
Ameongeza kuwa kwa sasa imempendeza Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kumhamishia katika Wilaya ya Muleba, hivyo anawatakia kila la heri katika kuijenga Pangani na Taifa kwa ujumla.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa