Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Bwa Isaya M Mbenje (mwenye miwani) akiambatana na Afisa Elimu Msingi, Bw Juma Mbwela wamekukagua Uwandikishaji na Uripoti wa Wanafunzi katika Shule mbalimbali Wilayani Pangani.
Zoezi hilo limefanyika Januari 8, 2024 ambapo Shule za Msingi na Sekondari zimeanza kupokea na kuandikisha wanafunzi wa Awali na Darasa la kwanza pamoja na wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2024.
Mkurugenzi ameendelea kutoa wito kwa Wazazi na Walezi kuwaandikisha watoto wenye umri wa kuanza masomo kwaajili ya kupata Elimu na kuwasisitiza wale wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kuripoti na kuanza masomo kwa muda uliopangwa.
Kwa upande wake Afisa Elimu Msingi Bw Juma Mbwela amesema kuwa Serikali chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeboresha mazingira ya kujifunzia ikiwemo kujenga Shule na kuboresha miundombinu ya kujifunzia, hivyo ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha anapeleka
mtoto Shule.
"Tayari mpaka sasa uripoti wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule zetu unaenda vizuri na Uandikishaji wa Darasa la kwanza na Awali upo hatua nzuri pia"
Miongoni mwa Shule zilizotembelewa ni pamoja na shule ya Msingi Mwera,shule ya Msingi Pangani,Shule ya Sekondari Funguni,Bushiri na Masaika ambapo hadi sasa uandikishaji upo hatua nzuri na uripoti wa wanafunzi upo vizuri na tayari kwa kuendelea na masomo yao.
#panganimpya
#Elimubora
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa