Maadhimisho hayo yamefanyika leo Agosti 7,2023, katika kata ya Mwera Wilayani Pangani na kuhudhuriwa na Mganga Mkuu Hospitali(W), Diwani wa Kata ya Mwera, Mwenyekiti wa Ccm Kata, Afisa Mtendaji, Mwenyekiti wa Kijiji na Wanakijiji wa kata hio, pamoja na Wataalamu mbalimbali kutoka hospitali ya Wilaya ya Pangani.
Wataalamu hao wametoa elimu ya Unyonyeshaji, wamefanya Tathmini ya hali ya lishe kwa watoto chini ya miaka mitano (5) kwa kutumia kamba ya MUAC, Kupima uwiano wa urefu kwa Uzito kwa watu wazima,kufanya mapishi ya mfano yenye kuzingatia Lishe bora.
Afisa Lishe (W) Ndg Daud Mwakabanje amesema kuwa maziwa ya mtoto ni muhimu kwani yana viini kinga vyenye faida kwa mtoto na kuwataka wazazi wanyonyeshe maziwa hayo ndani ya kipindi cha miezi 6 ili kuwezesha ukuaji bora na kuelimisha jamii juu ya unyonyeshaji bora kwa watoto ikiwemo kuacha kutumia simu wakati wa kunyonyesha kwani suala la unyonyeshaji ni suala la kihisia.
Aidha Afisa Tarafa wa kata ya Mkwaja Ndg, Shadrack George ambae amemuwakilisha mgeni rasmi Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amewapongeza wananchi kwa kujitokeza na kutoa rai kwa wakina mama kuendelea kuwanyonyesha maziwa watoto kadri wataalamu wa afya wanavyoelekeza.
Kwa upande wake mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Pangani Ndg, Ramadhani Hussein amesema kuwa, Unyonyeshaji wa Maziwa ya Mama kwa Mtoto yanafaida nyingi sana ikiwa ni pamoja na kuimarisha ukuaji bora kwa mtoto na amewapongeza pia kwani maendeleo ya lishe kwa watoto wao yapo vizuri. Ameongeza kuwa jambo la Lishe ni jambo la Kitaifa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesaini mikataba na wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi juu ya Lishe, hivyo tulichukulie kwa uzito kwaajili ya manufaa ya Taifa letu.
Maadhimisho ya Unyonyeshaji wa maziwa ya Mama kwa mtoto Duniani,yalianza tarehe 1.8.2023 chini ya kauli mbiu ya "Saidia Unyonyeshaji, Wezesha Wazazi kulea Watoto na Kufanya kazi zao kila Siku" na kuhitimishwa leo tarehe 07.08.2023.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa