Dondoo Muhimu kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji wa Maziwa ya Mama Duniani Agosti 1_ 7, 2025

- Mtoto mwenye umri wa mwezi 0-6, anyonyeshwe maziwa ya mama pekee isipokuwa mtoto akipata changamoto yoyote ya kiafya atatumia dawa au kitu chochote kwa ushauri wa Daktari.
- Mtoto asinyonyweshwe maziwa kwa kutumia chupa au chuchu bandia.
- Maziwa ya ng'ombe hayafai kwa matumizi ya mtoto mchanga
- Mtoto anyonyeshwe maziwa ya mama wakati wote anapohitaji
- Epuka kuweka alama ya mkasi wakati wa kumnyonyesha mtoto.
- Mwache mtoto anyonye ziwa moja mpaka atakapo tosheka ndipo umuhamishie ziwa lingine
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa