ELIMU YA MIKOPO YA ASILIMIA 10 YATOLEWA, JAIRA.
Leo, tarehe 9 Septemba 2024, Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mhe. Gift Isaya Msuya, ameongoza ziara ya kikazi katika kijiji cha Jaira, ambapo kipaumbele kilikuwa kutoa elimu kuhusu mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri kwa vikundi vya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu. Mikopo hii ni sehemu muhimu ya juhudi za serikali za kuinua kipato cha wananchi na kukuza maendeleo ya kiuchumi.
Katika ziara hiyo, Mhe. Gift alimtaka Afisa Maendeleo ya Jamii, Ndg. Rinus, kutoa maelezo ya kina kuhusu taratibu na masharti ya kupokea mikopo hiyo. Ndg. Rinus alisisitiza kuwa miongoni mwa sifa za kupokea mikopo hiyo ni pamoja na:
1. Kuwa na andiko la mradi linaloelezea malengo na matumizi ya mkopo.
2. Kutokuwa na ajira rasmi kwa wanakikundi.
3. Kikundi lazima kisajiliwe rasmi.
4. Wanachama wote wawe na namba ya NIDA.
Ndg. Rinus alisisitiza umuhimu wa vikundi kufuata taratibu zote muhimu katika kuomba mikopo hiyo, ili kuhakikisha wanapata fursa hii muhimu kwa maendeleo yao. Mikopo hii haina riba na inalenga kusaidia vikundi kuanzisha au kuimarisha miradi ya kijasiriamali, na hivyo kuchangia katika kuleta maendeleo endelevu katika jamii.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa