Halmashauri ya Wilaya ya Pangani kwa kushirikia na shirika lisilo lakiserikali la Afriwag wametekeleza kwa vitendo kampeni ya Gulio la Afya.
zoezi hilo lililo zinduliwa na Ndugu Marko Hupa afisa tarafa ya Mwera kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Pangani Mh. Mussa Kilakala.
Gulio hilo limefanyika leo Mei 29,2024, katika Kata ya Kipumbwi ambapo huduma mbalimbali za afya zimetolewa bure kwa wananchi wa eneo hilo. Huduma hizo zilijumuisha utoaji wa elimu na upimaji wa hali ya lishe kwa watoto na watu wazima(Kwa kuangalia uwiano wa urefu, uzito na miaka pamoja na kipimo cha muac), huduma za uzazi wa mpango iikiwemo elimu ya afya ya uzazi, ugawaji wa condom na njia nyingine za uzazi wa mpango, uchangiaji damu kwa hiari, elimu kuhusu ukatili wa kijinsia, upimaji hiari wa virusi vya UKIMWI, huduma za chanjo kwa watoto, elimu ya usajili wa Bima ya afya iliyoboreshwa (iCHF) na usjili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya siku 90.
Akiongea mara baada ya zoezi hilo mratibu wa gulio hilo kutoka shirika la Afriwag ndg Faraji Isiaka amesema kuwa _:
" Afriwag, kwa kushuirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Pangani tunaendelea kutembelea jamii ,vituo vya kutolea huduma ya afya,na kuwafikishia elimu ya kutosha ya namna gani ya kukabiliana na magonjwa na upimaji wa afya zao ”. alisema.
Kwa upande wake bi Patricia Mkude kutoka USAID AFYA YANGU MAMA NA MTOTO , amesema kuwa_:
"watumishi wa afya ngazi ya Jamii (CHW)wana umuhimu mkubwa katika kuhakikisha wanafikisha elimu ya afya katika maeneo yao".Alisisitiza.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa