Chuo cha Utalii cha Taifa,kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, wametoa mafunzo wezeshi kwa Vijana walio katika Mnyororo wa Utalii Wilaya ya Pangani.
Akifungua mafunzo hayo ya siku 5 yaliofanyika katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri lSeptemba 5,2023, Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mhe Zainab Abdallah Issa, ambae amehimiza kuendeleza utamaduni wa kuthamini na kuendeleza utalii uliopo Pangani
"Mungu ametupa neema ya kuwa karibu sana na Zanzibar pamoja na jiji la kibiashara la Dar es Salaam na Jiji la Utalii Arusha,hivyo tunapambana kuifufua Pangani ,tunaendelea kumshukuru Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha Pangani fedha za Miradi ya maendeleo na Mbunge wetu Jumaa Hamidu Aweso kwa kuendelea kutushika mkono wana Pangani". Sekta hii ya utalii inachangia asilimia 25 ya pato la Taifa hivyo ni sekta ya kimkakati".
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendajii Isaya Mbenje amesema kuwa mafunzo haya ni kuwajengea uwezo wa kuijua vizuri sekta ya utalii Vijana wa Pangani ili wazidi kuwa mabalozi wazuri wa Sekta hii ya Utalii Nchini Tanzania, ili kuweza kuutangaza utalii na Vivutio vyake vilivyopo kwa Ujumla.
Kwa upande wake mtoa mada kutoka chuo cha Taifa cha Utalii Tanzani bwan Roman Lasway amesema kuwa sekta ya Utalii inahitaji wataalam ili waweze kutoa huduma iliobora. Pangani yapo mazingira mazuri yenye kuvutia wageni hivyo Mafunzo haya ni muhimu sana kwani yatafungua dunia ya utalii kwa ujumla.
" Utalii ni moja kati ya sekta zinazoleta mapato kwenye nchi yetu, hivyo ni lazima tuilinde na tuitangaze kwa maslahi mapana ya Taifa letuMwenyekiti wa Halmashauri Akida Bahorera amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuendelea kuwakumbuka wakazi wa Pangani na kuwapa fursa hizi za maendeleo.
Wilaya ya Pangani ina vivutuo vingi vizuri vya utalii kama vile Mto Pangani wenye sifa ya pekee kama vile maji yake kukutana na Maji ya Bahari,mbuga bora ya Saadani,Mlima Mashado kuona mji wote wa Pangani, jiwe mwana unguja ,kisiwa cha Maziwe,na vivutio vingine vingi vyenye kuupendeza.
Vijana 20 watakao fanikiwa kufaulu vizuri mafunzo haya watapata nafasi ya kusoma mafunzo ya muda mrefu katika chuo cha Taifa cha Utalii, ili kuendeleza sekta ya Utalii Pangani.
#wekezapangani
#utaliinimali
#karibupangani
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa